Yakobo Mlango 1 James

Yakobo 1:1 James 1:1

Yakobo, mtumwa wa Mungu, na wa Bwana Yesu Kristo, kwa kabila kumi na mbili waliotawanyika; salamu.

Yakobo 1:2 James 1:2

Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;

Yakobo 1:3 James 1:3

mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi.

Yakobo 1:4 James 1:4

Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.

Yakobo 1:5 James 1:5

Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.

Yakobo 1:6 James 1:6

Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.

Yakobo 1:7 James 1:7

Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.

Yakobo 1:8 James 1:8

Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote.

Yakobo 1:9 James 1:9

Lakini ndugu asiye na cheo na afurahi kwa kuwa ametukuzwa;

Yakobo 1:10 James 1:10

bali tajiri kwa kuwa ameshushwa; kwa maana kama ua la majani atatoweka.

Yakobo 1:11 James 1:11

Maana jua huchomoza kwa hari, huyakausha majani; ua lake huanguka, uzuri wa umbo lake hupotea; vivyo hivyo naye tajiri atanyauka katika njia zake.

Yakobo 1:12 James 1:12

Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.

Yakobo 1:13 James 1:13

Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu.

Yakobo 1:14 James 1:14

Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.

Yakobo 1:15 James 1:15

Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.

Yakobo 1:16 James 1:16

Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike.

Yakobo 1:17 James 1:17

Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka.

Yakobo 1:18 James 1:18

Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limbuko la viumbe vyake.

Yakobo 1:19 James 1:19

Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika;

Yakobo 1:20 James 1:20

kwa maana hasira ya mwanadamu haiitendi haki ya Mungu.

Yakobo 1:21 James 1:21

Kwa hiyo wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, na kupokea kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu.

Yakobo 1:22 James 1:22

Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu.

Yakobo 1:23 James 1:23

Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo.

Yakobo 1:24 James 1:24

Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo.

Yakobo 1:25 James 1:25

Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.

Yakobo 1:26 James 1:26

Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai.

Yakobo 1:27 James 1:27

Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.