Yakobo Mlango 4 James

Yakobo 4:1 James 4:1

Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?

Yakobo 4:2 James 4:2

Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi!

Yakobo 4:3 James 4:3

Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.

Yakobo 4:4 James 4:4

Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.

Yakobo 4:5 James 4:5

Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu?

Yakobo 4:6 James 4:6

Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.

Yakobo 4:7 James 4:7

Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.

Yakobo 4:8 James 4:8

Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.

Yakobo 4:9 James 4:9

Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu.

Yakobo 4:10 James 4:10

Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza.

Yakobo 4:11 James 4:11

Ndugu, msisingiziane; amsingiziaye ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, huisingizia sheria na kuihukumu sheria. Lakini ukiihukumu sheria, huwi mtenda sheria, bali umekuwa hakimu.

Yakobo 4:12 James 4:12

Mtoa sheria na mwenye kuhukumu ni mmoja tu, ndiye awezaye kuokoa na kuangamiza. U nani wewe umhukumuye mtu mwingine?

Yakobo 4:13 James 4:13

Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida;

Yakobo 4:14 James 4:14

walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka.

Yakobo 4:15 James 4:15

Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi.

Yakobo 4:16 James 4:16

Lakini sasa mwajisifu katika majivuno yenu; kujisifu kote kwa namna hii ni kubaya.

Yakobo 4:17 James 4:17

Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi.