Yakobo Mlango 2 James

Yakobo 2:1 James 2:1

Ndugu zangu, imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwe nayo kwa kupendelea watu.

Yakobo 2:2 James 2:2

Maana akiingia katika sinagogi lenu mtu mwenye pete ya dhahabu na mavazi mazuri; kisha akiingia na maskini, mwenye mavazi mabovu;

Yakobo 2:3 James 2:3

nanyi mkimstahi yule aliyevaa mavazi mazuri, na kumwambia, Keti wewe hapa mahali pazuri; na kumwambia yule maskini, Simama wewe pale, au keti miguuni pangu,

Yakobo 2:4 James 2:4

je! Hamkufanya hitilafu mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo mabovu?

Yakobo 2:5 James 2:5

Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?

Yakobo 2:6 James 2:6

Bali ninyi mmemvunjia heshima maskini. Je! Matajiri hawawaonei ninyi na kuwavuta mbele ya viti vya hukumu?

Yakobo 2:7 James 2:7

Hawalitukani jina lile zuri mliloitwa?

Yakobo 2:8 James 2:8

Lakini mkiitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa, Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vema.

Yakobo 2:9 James 2:9

Bali mkiwapendelea watu, mwafanya dhambi na kuhukumiwa na sheria kuwa wakosaji.

Yakobo 2:10 James 2:10

Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.

Yakobo 2:11 James 2:11

Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria.

Yakobo 2:12 James 2:12

Semeni ninyi, na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru.

Yakobo 2:13 James 2:13

Maana hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma. Huruma hujitukuza juu ya hukumu.

Yakobo 2:14 James 2:14

Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! Ile imani yaweza kumwokoa?

Yakobo 2:15 James 2:15

Ikiwa ndugu mwanamume au ndugu mwanamke yu uchi na kupungukiwa na riziki,

Yakobo 2:16 James 2:16

na mtu wa kwenu akawaambia, Enendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, lakini asiwape mahitaji ya mwili, yafaa nini?

Yakobo 2:17 James 2:17

Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake.

Yakobo 2:18 James 2:18

Lakini mtu atasema, Wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa njia ya matendo yangu.

Yakobo 2:19 James 2:19

Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka.

Yakobo 2:20 James 2:20

Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai?

Yakobo 2:21 James 2:21

Je! Baba yetu Ibrahimu hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu?

Yakobo 2:22 James 2:22

Waona kwamba imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, na ya kwamba imani ile ilikamilishwa kwa njia ya matendo yale.

Yakobo 2:23 James 2:23

Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu.

Yakobo 2:24 James 2:24

Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake.

Yakobo 2:25 James 2:25

Vivyo hivyo na Rahabu, yule kahaba naye, je! Hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia nyingine?

Yakobo 2:26 James 2:26

Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.