Yona Mlango 2 Jonah

Yona 2:1 Jonah 2:1

Ndipo Yona akamwomba Bwana, Mungu wake, katika tumbo la yule samaki,

Yona 2:2 Jonah 2:2

Akasema, Nalimlilia Bwana kwa sababu ya shida yangu, Naye akaniitikia; Katika tumbo la kuzimu naliomba, Nawe ukasikia sauti yangu.

Yona 2:3 Jonah 2:3

Maana ulinitupa vilindini, Ndani ya moyo wa bahari; Gharika ya maji ikanizunguka pande zote; Mawimbi yako yote na gharika zako zote zimepita juu yangu.

Yona 2:4 Jonah 2:4

Nami nikasema, Nimetupwa mbali na macho yako; Lakini nitatazama tena kukabili hekalu lako takatifu.

Yona 2:5 Jonah 2:5

Maji yalinizunguka, hata nafsini mwangu; Vilindi vilinizunguka; Mwani ulikizinga kichwa changu;

Yona 2:6 Jonah 2:6

Nalishuka hata pande za chini za milima; Hiyo nchi na mapingo yake yalinifunga hata milele; Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka shimoni, Ee Bwana, Mungu wangu,

Yona 2:7 Jonah 2:7

Roho yangu ilipozimia ndani yangu, Nalimkumbuka Bwana; Maombi yangu yakakuwasilia, Katika hekalu lako takatifu.

Yona 2:8 Jonah 2:8

Watu waangaliao mambo ya ubatili na uongo Hujitenga na rehema zao wenyewe;

Yona 2:9 Jonah 2:9

Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani; Nitaziondoa nadhiri zangu. Wokovu hutoka kwa Bwana.

Yona 2:10 Jonah 2:10

Bwana akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona pwani.