Chorus / Description :
Nikumbushe wema wako nisije laumu
Nikumbushe ukuu wako wakati wa Magumu
Nikumbushe shuhuda zako ili nikusifu
Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machozi
Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machozi,
Nirahisi kinywa kujawa na lawama tele
Pale mambo yanapoonekana hayaendi
ni ajabu sana namna moyo unahangaika
Ajabu sana moyo unavyoonyesha mashaka yakwamba
japokuwa Mungu anaishi ndani yangu kuna muda nahofu,
Japokuwa Mungu anaketi kati yetu kuna muda nahofu, ahh
nakumbuka wana wa Israel katika bahari yashamu
Japo walikatiza katikati ya bahari kwa ushindi,
Kwa nyimbo nyingi waliimba na kumsifu Bwanaa.
Lakini baada ya kuvuka na kuliona jagwa
yalibadilika mambo, manung'unikoo yalisimama
Na kusahau muujiza alotenda Bwana Mwanzo aah.
Eee MUNGU Nisaidie ee eeh
Nikumbushe wema wako nisije laumu
Nikumbushe ukuu wako wakati wa Magumu
Nikumbushe shuhuda zako ili nikusifu
Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machozi,
Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machozi,
Eeh ee MUNGU Nisaidie
Nisaidie kukumbuka baba yakwamba umenichora
Kiganjani mwako kati ya wengi walioko duniani eenh
na mimi umenionaa oooh ooo
Nikumbushe baba yakwamba ni wewe umeniponya nilipoumwa
Yakwamba ni wewe mlipaji wa ada yangu shuleni.
ouoh ooh Yakwamba kama ungeniacha hatua moja
nisingelifika nilipo ooh eee Babaa
umenikung'uta mavumbi, kung'uta
mavumbi mimi na kuniheshimisha.
Nikumbushe wema wako nisije laumu
Nikumbushe ukuu wako wakati wa Magumu
Nikumbushe shuhuda zako ili nikusifu
Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machozi
Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machozi,
Nikumbushe wema wako nisije laumu
Nikumbushe ukuu wako wakati wa Magumu
Nikumbushe shuhuda zako ili nikusifu
Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machozi
Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machozi,
Yesu nakutazama ninakuamini wewe
Fungua maisha yangu, nisaidie nisilalamike
Mbele zako, katika hali zote nijue upo
Umesema hutaniacha eeh Yahweh