Beda Andrew - Nitakuwa Na Wewe

Chorus / Description : Sababu ninaelewa nikiwa na wewe napata raha
Ninaelewa kuishi na wewe ni furaha
Ninelewa iyee ninaelewa oooh

Hata iweje wafanyeje wasemeje
Mimi sitakuacha
Hata iweje wafanyeje wasemeje mimi sitakuacha
Nitakuwa na wewe (iyee)
Nikae na wewe (iyee)
Nitembee na wewe (milele)
Mwokozi wangu

Nitakuwa Na Wewe Lyrics

Kama ni kukupenda niko sawa 
Kuwa nawe niko sawa 
Niko tayari walimwengu wanitenge 
Kama kuwa nawe ni kushamba 
Kuishi nawe si kujanja 
Niko tayari walimwengu wanicheke 

Sababu ninaelewa nikiwa na wewe napata raha 
Ninaelewa kuishi na wewe ni furaha 
Ninelewa iyee ninaelewa oooh

Hata iweje wafanyeje wasemeje 
Mimi sitakuacha 
Hata iweje wafanyeje wasemeje mimi sitakuacha 
Nitakuwa na wewe (iyee) 
Nikae na wewe (iyee) 
Nitembee na wewe (milele) 
Mwokozi wangu 

Maneno neno ya wanadamu yanavunja moyo yanapotosha 
Dhumuni lake ni kunitenga mbali nawe 
Kwa damu uliyo mwaga msalabani ili mimi niwe wathamani 
Sio rahisi kwa mwanadamu kunitenga nawe  

Kwangu ninaelewa nikiwa na wewe napata raha 
Ninaelewa kuishi na wewe ni furaha 
Ninelewa iyee ninaelewa oooh 

Hata iweje wafanyeje wasemeje 
Mimi sitakuacha 
Hata iweje wafanyeje wasemeje mimi sitakuacha 
Nitakuwa na wewe (iyee) 
Nikae na wewe (iyee) 
Nitembee na wewe (milele) 
Mwokozi wangu 

Moyo wangu nimekukabidhi 
Na mwili wangu hekalu lako 
Wewe Bwana nimekubali ukae nami 
Nitakuwa nawe siku zote 
Milele na milele sitokuacha 
Nitakubali kuacha vyote nikufuate wewe 
Sababu ninaelewa, ninaelewa 
Ninaelewa 

Nitakuwa na wewe (iyee) 
Nikae na wewe (iyee) 
Nitembee na wewe (milele) 
Mwokozi wangu 

Nitakuwa Na Wewe Video

  • Song: Nitakuwa Na Wewe
  • Artist(s): Beda Andrew


Share: