Chorus / Description :
ningekuwa wapi, kama si wewe
ningeitwa nani, kama si wewe
ningefanya nini, kama si wewe
kwani bila wewe, mimi si kitu
Pendo gani hili, bwana ukanipenda
kabla nikujue, wewe umenipenda
mimi nani sasa, bila wewe maishani
kabla nikujue, wewe ulinipenda
na wakati nakukosea, Bwana wee wanisamehe
waniita mwana wako, hata wakati ni dhaifu
sistahili mbele zako, naja kwa unyenyekevu
kwani mimi bila wewe, mimi si kitu, si kitu
ningekuwa wapi, kama si wewe
ningeitwa nani, kama si wewe
ningefanya nini, kama si wewe
kwani bila wewe, mimi si kitu
nikikumbuka jinsi ulivyo,sina la kusema
nilipotea, kwenye dhambi ukaniokoa
mimi ni nani, mbele zako
kama sio wewe,ningekuwa wapi
kama si wewe,ulinipenda
ukanionyesha njia.ulinipenda
ukaniokoa sina mwingine
ningekuwa wapi, kama si wewe
ningeitwa nani, kama si wewe
ningefanya nini, kama si wewe
kwani bila wewe, mimi si kitu
najitoa kwako bwana, uinuke ndani yangu
mimi kwako mtumishi, nitumie upendavyo
najitoa kwako bwana,nitumie upendavyo
mimi kwako mtumishi, nakuomba nitumie
nijaze, nijaze, nijaze na roho yako
nifinyange, nitumie, najitoa mbele zako
ningekuwa wapi, kama si wewe
ningeitwa nani, kama si wewe
ningefanya nini, kama si wewe
kwani bila wewe, mimi si kitu
@ Billy Frank & Mercy Wairege
Kama Si wewe (Were it not for You)