Boaz Danken - Ninakushukuru

Chorus / Description : Ninakushukuru kwa yale uliyoyafanya jana
Ninakushukuru kwa yale unayafanya leo
Ninakushukuru kwa yale utakayoyafanya kesho
Maana miaka yangu dunia imehesabiwa na wewe

Ninakushukuru Lyrics

Nimekuja mbele zako ili nikushukuru 
Wewe ndiwe kila kitu kwangu mimi nakushukuru 
Nimekuja mbele zako ili nikushukuru 
Wewe ndiwe kila kitu kwangu mimi nakushukuru 
Nimekuja mbele zako ili nikushukuru 
Wewe ndiwe kila kitu kwangu mimi nakushukuru 

Ninakushukuru kwa yale uliyoyafanya jana 
Ninakushukuru kwa yale unayafanya leo 
Ninakushukuru kwa yale utakayoyafanya kesho 
Maana miaka yangu dunia imehesabiwa na wewe
(repeat)

Asante kwa mawazo mazuri kwangu 
Yananipa tumaini siku ya mwisho 
(repeat)

Ningeamka asubuhi bila wewe Mungu wangu 
Pale nilipolala usingizi huku nikikata tamaa 
Ukaituma hekima kwa siri moyoni mwangu 
Ukanikumbusha agano na uaminifu wako 
Ukautuma wimbo wa sifa moyoni mwangu 
Ili nikusifu na kukushukuru 

Ninakushukuru kwa yale uliyoyafanya jana 
Ninakushukuru kwa yale unayafanya leo 
Ninakushukuru kwa yale utakayoyafanya kesho 
Maana miaka yangu dunia imehesabiwa na wewe
(repeat)

Asante Bwana kwa wema na fadhili zinazodumu milele 
Asante Bwana kwa wema na fadhili zinazodumu milele 
Asante Bwana kwa wema na fadhili zinazodumu milele 

Ninakushukuru Video

  • Song: Ninakushukuru
  • Artist(s): Boaz Danken
  • Album: Ninakushukuru (Live) - Single
  • Release Date: 17 Sep 2020
Ninakushukuru Audio Preview: Download / Stream : Amazon Music / iTunes
Ninakushukuru

Share: