Chorus / Description :
Njoo ufanyiwe maombi (Njoo uombewe)
Njoo ufanyiwe maombezi mama
Njoo ufanyiwe maombi (kwa jina la Yesu kristo)
Njoo ufanyiwe maombezi baba
Ukiombewa tatizo lako kidogo (kidogo)
Ukiombewa tatizo lako kidogo hilo
Njoo ufanyiwe maombi
Njoo ufanyiwe maombezi baba
Njoo njoo njoo ooh
Njoo kaka njoo baba, njoo mama njoo oh
Tatizo lako umezunguka nalo sana
Sehemu nyingi umezunguka
Kwa Yesu sasa njooo (Njoo mama)
Njoo ufanyiwe maombi (Njoo uombewe)
Njoo ufanyiwe maombezi mama
Njoo ufanyiwe maombi (kwa jina la Yesu kristo)
Njoo ufanyiwe maombezi baba
Ukiombewa tatizo lako kidogo (kidogo)
Ukiombewa tatizo lako kidogo hilo
Njoo ufanyiwe maombi
Njoo ufanyiwe maombezi baba
Nazunguka mitaani natangaza Yesu ni Bwana
Kwa wagonjwa mbalimbali nawaambia Yesu anaweza
Na wewe unayenisikia nasema Yesu ndiye mthibitisha
Na wewe unayenisikia leo nasema Yesu nina uhakika naye
Njoo ufanyiwe maombi
Huu ndio ushauri wangu kwako
Njoo ufanyiwe maombi
Wenye tatizo kama lako
Wengi walishafunguliwa
Njoo ufanyiwe maombi (Njoo uombewe)
Njoo ufanyiwe maombezi kaka
Njoo ufanyiwe maombi (wengi wameombewa)
Njoo ufanyiwe maombezi baba (Usiteseke bure)
Ukiombewa tatizo lako kidogo
Ukiombewa tatizo lako kidogo hilo
Yesu ni mwanaume Kati ya wanaume
Yesu ni mwanaume eeh
Hili tatizo la kupata ajira
Limekuwa sugu kwako
Vyeti unavyo na sifa za kupa kazi unazo
Lakini roho ya kukatiliwa inakusumbua
Mfanya biashara unayenisikia
Huwezi kufanya lolote bila Mungu eeh
Biashara yako ilete kwa Mungu
Kwani yeye ndiye chanzo cha mafanikio
Akuepushe na kina chuma ilete
Biashara yako iwe na mafanikio
Njoo ufanyiwe maombi
Huu ndio ushauri wangu kwako
Njoo ufanyiwe maombi (Njoo uombewe)
Njoo ufanyiwe maombezi kaka
Njoo ufanyiwe maombi (wengi wameombewa)
Njoo ufanyiwe maombezi baba
Ukiombewa tatizo lako kidogo
Ukiombewa tatizo lako kidogo hilo
Mwilini mwako unahisi kuna vitu vinatembea
Madaktari hawalioni tatizo
Tatizo hili linakuchanganya pole
Waganga hawaliwezi tatizo hilo
Tatizo hili linakuchanganya pole
Waganga hawaliwezi tatizo hilo
Njoo ufanyiwe maombi
Huu ndio ushauri wangu kwako
Njoo ufanyiwe maombi (Njoo uombewe)
Njoo ufanyiwe maombezi dada
Njoo ufanyiwe maombi (wengi wameombewa)
Njoo ufanyiwe maombezi ndugu yangu wee
Ukiombewa tatizo lako kidogo
Ukiombewa tatizo lako kidogo hilo