Christina Shusho - Teta Nao Remix

Chorus / Description : Eeh Bwana utete nao wanaoteta nami
Upigane nao wanaopigana nami
Eeh Bwana utete nao wanaoteta nami
Upigane nao wanaopigana nami

Teta Nao Remix Lyrics

Eeeh Bwana utete nao wanao teta nami 
Upigane nao wanao pigana nami 
Eeeh Bwana utete nao wanao teta nami 
Upigane nao wanao pigana nami 
Ushike ngao na kinga usimame nami unisaidie 
Vuta we mkuki uwapige wanaonifuatia 
Uambie nafsi yangu mimi ni wokovu wako 
Wananiuliza mambo nisiyoyajua 

Eeh Bwana utete nao wanaoteta nami 
Pigana nao wanaopigana nami 
Eeh Bwana utete nao wanaoteta nami 
Pigana nao wanaopigana nami 

Wahaibishwe wafedheheshwe 
Warudishwe nyuma wanaotafuta nafsi yangu 
Wafadhaishwe wawe kama makapi 
Mbele yao pepo malaika wa Bwana waangushe chini Wananilipa mabaya badala ya mema 
Kutwa kucha waniwinda ili niteseke ee 
Niko ndani yako niweke eeh Mungu 
Ubavuni mwako nikumbatie Jehovah wangu 
Mkononi mwako niweke eeh Mungu 
Ubavuni mwako nikumbatie Jehovah wangu 

Eeh Bwana utete nao wanaoteta nami 
Upigane nao wanaopigana nami 
Eeh Bwana utete nao wanaoteta nami 
Upigane nao wanaopigana nami 

Njia yao iwe giza na utelezi 
Malaika wa Bwana akiwafuatia 
Uharibifu uwapate kwa ghafla  
Wa uharibifu aanguke ndani yake 
Mimi bure wasinisemange bure wasinibonge 
Na uovu wao aloficha umnase mwenyewe 
Bila sababu amenichimbia shimo nafsi yangu 
Mifupa yangu yote itasema 
"Bwana ni nani aliye kama wewe?" 
Na nafsi yangu itamfurahia Bwana 

Wapendeza Bwana wapendeza eeh Bwana wapendeza 
Katika hili najua utatenda 
Nitetee Bwana nitetee eeh Bwana nitetee 
Katika hili najua utatenda 

Teta Nao Remix Video

  • Song: Teta Nao Remix
  • Artist(s): Christina Shusho


Share: