Chorus / Description :
Ninapoonewa ninapolemewa
Giza likitanda nuru zikiisha
Mungu wangu nisaidie
Mateso yakizidi hofu hutawala
Hakuna tumaini lini yatakwisha
Imani yatoweka hakuna tumaini
Mungu wangu nisaidie
Hakuna hata moja aniwazia mema
Adui wamezidi rafiki wageuka
Sioni hata moja wakunisaidia
Baba wee Mungu wangu nisaidie
Ninapoonewa ninapolemewa
Giza likitanda nuru zikiisha
Mungu wangu nisaidie
Mungu nakungoja wewe
Nipe nguvu mpya
Nivuke kama tai
Nitembee bila kuchoka
Nipige mbio mbele bila kuzimia
Mungu wangu nisaidie
Nimeshajinyonyoa manyoya
Nimeparua kwa mbali
Nimepunguza uzito kwa bidii
Niko tayari kuruka tena
Maisha yangu ya pili nzuri
Kulinganisha na yale ya kwanza
Niko tayari ninazo nguvu kama tai
Ujana wangu umerejea
Maisha yangu yamerejea
Sasa niko na nguvu
Sioni wii tena haleluya
Ninapoonewa ninapolemewa
Giza likitanda nuru zikiisha
Mungu wangu nisaidie
Nisaidie nisaidie
Nisaidie nisaidie
Wale wangojao watapata nguvu mpya
Watapaa juu kwa mbali kama tai
Ninapoonewa ninapolemewa
Giza likitanda nuru zikiisha
Mungu wangu nisaidie
Mungu wangu nisaidie
Ninapoonewa ninapolemewa
Giza likitanda nuru zikiisha
Mungu wangu nisaidie