Chorus / Description :
Hauwezi Kushindana Oh Kushindana
Na mwanadamu mwenye kinywa ayayaya
Hauwezi Kushindana Oh Kushindana
Na mwanadamu mwenye kinywa ayayaya
Hauwezi Kushindana Oh Kushindana
Na mwanadamu mwenye kinywa ayayaya
Hauwezi Kushindana Oh Kushindana
Na mwanadamu mwenye kinywa ayayaya
Kama maneno yangekuwa yanaweza kutoboa mwili huu
Mbona sasa ngingekuwa na vidonda mwili mzima
Vita ya maneno kuna watu majemedari
Ukisema mshindane mbona mikono utainua
Kupigwa vita ni kawaida isikusumbue
Wewe ni mti wenye matunda zoea mawe
Lia kidogo nyamaza ili uchungu uishe
Ukiendelea unawapa kichwa hawa
Vaa silaha za imani rejea vitani
Wakikuona waseme umeshakua sugu
Acha waonge acha waseme seme
Ila yupo Mungu wakuwaziba Midomo
Hauwezi Kushindana Oh Kushindana
Na mwanadamu mwenye kinywa ayayaya
Hauwezi Kushindana Oh Kushindana
Na mwanadamu mwenye kinywa ayayaya
Ikiwa Mungu anahukumu kwa kuskiza maneno
Mbona hata matumbo ya mimba yanasemwa sana
Hivi Mungu angehukumu kwa kuskiza umbeya
Si ningekushauri mchungaji wangu ufunge kanisa
Mwanadamu mwanadamu shida ni ulimi
Ungejifunza ukimya haunanga hasara
Fulani we fulani unashida gani, na uongo wa nini?
Mwogope Mungu, ukumbuke ni ahadi kuna siku yaja
Kwa kila neno la kinywa chako utatolea hesabu
Mimi si Nimeshakwambia kubali uache
Utajijua na shingo yako ngumu ayaya
Siwezi kushindana, na mwanadamu mwenye kinywa
Hauwezi Kushindana Oh Kushindana
Na mwanadamu mwenye kinywa ayayaya
Hauwezi Kushindana Oh Kushindana
Na mwanadamu mwenye kinywa ayayaya
Yesu huyu Yesu Hakujitetea kabisa
Japo walimsema kwa ubaya aliwasamehe
Na wewe uwasamehe uwaombee kwa maana hawajui wasemayo
Wakifanyanga ubaya uwajibu kwa wema
Usishindane na mtu wajibu kwa wema
Hata iwe ni ndugu wa karibu wajibu kwa wema
Si vizuri wewe usilipe kisasi
Wajibu kwa wema
Tenda wema uende
Wajibu kwa wema
ah ah ah, wajibu kwa wema
oh maana maana
Hauwezi Kushindana Oh Kushindana
Na mwanadamu mwenye kinywa ayayaya
Hauwezi Kushindana Oh Kushindana
Na mwanadamu mwenye kinywa ayayaya