Goodluck Gozbert - Mpaka Lini

Chorus / Description : Mpaka lini?
Baba mpaka lini !
Maisha ya mateso, mpaka lini
masimango, mpaka lini
Kuonewa onewa, mpaka lini?
Baba mpaka lini mpaka

Mpaka Lini Lyrics

Jana nilimkuta kijana mmoja, amejiinamia amekata tamaa.
Mkono wa kushoto ameshika kilevi,
Na huku wa kulia msokoto wa bangi,
Nikamuuliza nini uko hivi, amekataa tamaa.
Aliniangalia nikaona kitu machoni mwake
Alikuwa mtu wa huzuni nyingi.
Nikamwambia kwa nini unanung'unika mpendwa.
Hivi unajua Yesu anakupenda
Alichonijibu ah alichonieleza kinawatesa wengi
" Yani kama ni matatizo nahisi sasa mimi ndo nimeamka nayo
na nashinda nayo na nitalala nayo na kesho asubuhi nitaamka nayo
aah Mungu kwa kweli Mungu wangu hapana"

Akaniambia
"Huwa nakumbuka siku niliyozaliwa nilimlaumu mama
pengine ndio chanzo cha haya Yote
Najiuliza nilimkosea nini Mungu hata iwe hivi.
Mama yangu mjane nyumba yetu kila siku mikosi, aa Why??

Pindi nipo shuleni nafukuzwa bila sababu yoyote
Lakini kikubwa nahisi itakuwa umasikini.
Nikasema Why? labda ningekuwa mvuvi.
Lakini bado ni ugumu wa maisha
Ndugu zangu niliowategemea wangenikumbuka
Hawataki hata kuniona, ona wadogo zangu wanafanikiwa
mimi ni masikini. Why ?? Hata na mke wangu hashiki ujauzito Why?
Hospitali nimemaliza waganga nimemaliza lakini sioni hata dalili
Huyo ni Mungu wenu labda anawasikia ninyi tu. Sisi hatujali..

Nikasema labda niokoke nimpokee Yesu
Shida zitaniisha nitakuwa huru kabisa
Cha ajabu wapendwa hawaishi kunisema WHY?
Nimeteseka sana, nachohisi labda milango yangu
Ya baraka imefungwa Why?
Kama si hivyo basi nina laana ya ukoo
Mbona matatizo na mimi ___ na mimi

Mpaka lini mpaka lini mpaka lini ?
Baba mpaka lini
Maisha ya mateso, mpaka lini
masimango, mpaka lini
Kuonewa onewa, mpaka lini?
Baba mpaka lini mpaka

Mpaka Lini Video

  • Song: Mpaka Lini
  • Artist(s): Goodluck Gozbert


Share: