Goodluck Gozbert - Shukurani

Chorus / Description : Shukurani zangu kwako nashukuru.
Shukurani zangu kwako Baba
Asante, Shukurani zangu kwako nashukuru.
Shukurani zangu kwako Baba

Shukurani Lyrics

Ninakushukuru Mungu sababu ya bei
Hata uhai sikustahili
Ninakushukuru Mungu tena sababu ya dhiki
ata nikisali unajua namaanisha
Siokama eti nilitenda wema kwa kujalisha matendo yako makuu
Mimi Mungu ningekulipa nini. Ulikonitoa nisinge moyo wangu
matopeni topeni ukaniketisha na wakuu.
Umenipaa heshima ukanifuta machozi asante ooh Baba.

Hata shukurani zangu kwako nashukuru.
Shukurani zangu kwako Baba

Aibu umefuta, fedheha umevuta, umenipa amani iliyo ya kweli.
Nakumbuka ndani yangu mimi ndo yule amabaye
nilitoka na kwa dharau kwisha hai.
Kuna kipindi nilikufa nikawa mifupa inayotembea.
Ikiwa kwa siku za usoni wakasema tunazika kesho.
Ila kwa huruma uliniponya na kaburi
Kwa huruma sitosahau wema wako wee.

Shukurani zangu kwako nashukuru.
Shukurani zangu kwako Baba
Asante, Shukurani zangu kwako nashukuru.
Shukurani zangu kwako Baba

Kama ni kusoma tulisoma wengi umeruhusu niwe na kazi nzuri.
Ajali tulipata wengi umeruhusu nibaki na uzima
Ndoa zimefungwa nyingi umeruhusu tubaki na amani.
Furaha walikosa wengi umeruhusu tabasamu kwangu

Na Shukurani
yelele Mama, yelele mama, yelelele
yelele Mama, yelele mama, yelelele
yelele Mama, yelele mama, yelelele
yelele Mama, yelele mama, yelelele



Shukurani Video

  • Song: Shukurani
  • Artist(s): Goodluck Gozbert


Share: