Chorus / Description :
Hadithi hadithi njoo
Ukitenda mema unajitendea mwenyewe
Ukitenda maovu unajitendea mwenyewe
Hadithi hadithi njoo
Hadithi hadithi njoo
Hadithi hadithi njoo
Verse 1
Kuna bwana mmoja wa kichaa
alipenda kuomba chakula kwa mama fulani, mama fulani.
Siku moja yule mama alipanga amtilie sumu,
yule wazimu akila afe aondoke kabisa,
kule njiani alipatana na watoto wa yule mama akawagawanyiaa kile chakula.
Watoto wake wakala wakafa, yule wazimu akabaki mzima
ishara kwamba unayo yatenda unajitendea mwenyewe X 2
Chorus
Ukitenda mema unajitendea mwenyewe
Ukitenda maovu unajitendea mwenyewe X 2
Verse 2
Salimia watu pesa huisha
Gari hupata puncture hivi ni vitu vya dunia,
hichi kidole nacho wanyoshea watu. Vingine vinne ninajinyoshea mwenyewe X 2
Ninaozungumza nao juu ya wenzangu, wanazungumza nao juu yangu mimi X 2
Tenda mema ondoka uende alo na chuki na wewe mpende kwasababu unayo yatenda unajitendea mwenyewe*2
Chorus
Ukitenda mema unajitendea mwenyewe
Ukitenda maovu unajitendea mwenyewe X 2