Chorus / Description :
Huu wimbo ninaimba oh, sio wimbo ni maombi
Nikiomba Mwenyezi Mungu oh aibariki Kenya yangu
kwa jina la Baba na la Mwana oh, Roho Mtakatifu Amina
Ewe Kenya nchi yangu, ewe Kenya baba yangu
Ewe Kenya mama yangu oh, sitakuwacha milele

Akili zangu, nguvu zangu oh, nimeziweka mbele yako
Bibi yangu na watoto oh, nimewaweka mbele yako
Taabu zangu, shida zangu oh, ziangalie Kenya yangu
Taabu zangu, shida zangu oh, ziangalie Kenya yangu
Ewe Kenya nchi yangu, ewe Kenya baba yangu
Ewe Kenya mama yangu oh, sitakuwacha milele
Matajiri maskini oh, sisi sote binadamu
Matajiri maskini oh, sisi sote binadamu
Tusahau majivuno oh, na tuwache kupayuka

Utajiri, majivuno oh, sio tikiti ya mbinguni
Bahati yako ni ya leo ile ya kesho ndio yangu
Ewe Kenya nchi yangu, ewe Kenya baba yangu
Ewe Kenya mama yangu oh, sitakuwacha milele
Mhalifu twakujua mharibu twakuona tu
Plan zako twazijua lengo lako twalijua tu
Wataka kunyamba Kenya we utuharibie hewa
Harufu yako twaijua hata ukipanda ndege
Ewe Kenya nchi yangu, ewe Kenya baba yangu
Ewe Kenya mama yangu oh, sitakuwacha milele
...
A Patriotic Kenyan Song to Thank The Almighty especially on national
days such as Jamhuri/independence Day.