Martha Mwaipaja - Muhukumu Wa Haki

Chorus / Description : Hapo ndipo falme zote za dunia zitanyamaza
Mwenye wa kweli atawala
Atasimamia mahakama zote kwa haki
Atasimamia kesi zote kwa haki
Kila mmoja atalipwa sawa

Muhukumu Wa Haki Lyrics

Parapanda itapigwa itapigwa 
Parapanda itasika itasikika 
Hapo ndipo mfalme wa haki atakapotawala 
Hapo ndipo mfalme wa kweli atakapotawala 
Maana dunia ya leo watu wanabebeana 
Maana dunia ya leo watu wanapendeleana
Atatawala mwenye dunia 
Maana dunia ya leo watu wanapendeleana 

Hapo ndipo falme zote za dunia zitanyamaza 
Mwenye wa kweli atawala 
Atasimamia mahakama zote kwa haki 
Atasimamia kesi zote kwa haki 
Kila mmoja atalipwa sawa 

Dunia yote itatiishwa kwenye uweza wake 
Dunia yote itashangaa alivyo wa haki 
Mataifa watajua yeye ni mwema 
Hapo ndipo wote tutajua yeye ni baba 
Dunia yote itaelewa ni Mungu wa haki 
Maana dunia ya leo watu wanasaidiana 
Maana dunia ya leo watu wanasaidiana 
Atatawala asiyejua pendelea mwingine 
Watu wa leo wanatazama sifa ya mtu 

Majira yanakuja ya kujua baba wa kweli 
Majira yanafika watamjua Mungu wetu 
Leo hawatambua machozi tunayolia 
Leo hata ukilia hakuna wa kutazama 
Hata ukiteswa hakuna wa kutazama 
Wakati unapo janga atatawala kwa haki 
Hapo ndipo falme zitajua yeye ni mfalme 
Hapo ndipo dunia itaelewa yeye ni Bwana 

Tutapanguzwa machozi yetu na sisi 
Tutaheshimiwa na dunia na sisi 
Tutaheshimiwa na watu wote na sisi 
Hawawezi tambua haki yako leo hii 
Maana dunia ya leo watu wanasaidiana 
Hakuna wa kutetea maisha yangu 
Watawala wa leo wanapendeleana 
Anakuja mtawala wa haki kutusaidia 
Utarahi na Baba 
Tutashangilia kwa Baba 
Maana ufalme wake Baba utakuwa ni wenye haki 
Baba yetu akitawala 

Atatawala haaa 
Atatawala haaa 
Atatawala haaa 
Atatawala haaa 
...

  • Song: Muhukumu Wa Haki
  • Artist(s): Martha Mwaipaja
Muhukumu Wa Haki

Share: