Martha Mwaipaja - Naiona Kesho

Chorus / Description : Naiona kesho kesho
Iliyopangwa na Baba
Naiona kesho kesho
Iliyopangwa na Mungu

Naiona Kesho Lyrics

Naiona kesho kesho
Iliyopangwa na Baba 
Naiona kesho kesho
Iliyopangwa na Mungu  .

Naiona kesho mimi kesho iliyopangwa na Baba 
Kesho ya heshima aah iliyopangwa na Baba 
kesho ya Neema iliyopangwa na Baba 
Kesho yenye utukufu iliyopangwa na
Baba kesho ya kuinuliwa iliyopangwa na Baba 
Kesho ya ushindi ii iliyopangwa na Mungu
Kesho yenye nguvu iliyopangwa na Baba  .

Sitaki kuitazama leo yangu mwenzenu
Leo yangu ni shida mwenzenu
Leo yangu ni tabu mwenzenu
Leo machozi yanitoka aah mwenzenu 
Leo nimekataliwa aah mwenzenu
Leo nimefukuzwa mapema mwenzenu 
Leo wote waniacha aah mwenzenu 
Leo machozi ni mengi hii mwenzenu  .

Sitaki kuitazama Leo yangu kamwe
Sitaki kuitazama Leo yangu mimi 
Leo yangu ninalia mwenzenu
Leo ninateseka aah mwenzenu
Leo mateso ni mengi hii mwenzenu .

Naiona kesho yangu mwenzenu 
Naiona kesho yangu mwenzenu  .

Japo vita yangu ni kubwa mwenzenu 
Maadui wangu ni wengi mwenzenu 
Japo mateso yangu ni magumu mwenzenu 
Kuna neno amesema nami mwenzenu 
Atapigana aah amesema 
Atafanya mlango ooh amesema 
Atanifanyia wepesi amesema  .

Japo vita yangu kubwa mwenzenu 
Japo adui ni wengi mwenzenu 
Japo njia siioni mwenzenu 
Atapigana mwenyewe amesema 
Atafanya wepesi iiih amesema 
Atanifanyia wepesi kwani amesema 
Atanichunga salama amesema 
Atafanya mlango ooh amesema 
Atapigana na adui aah amesema   .

Kasema niione kesho aliyoniwekea 
Kasema niione kesho aliyoniwekea  .

Kuna majira yalifika nikajua Mungu
Kuna majira yalifika nikamwelewa
Majira Yale yalikuwa magumu 
Majira Yale yalikuwa magumu  .

Kwa macho yangu nikaona akitenda 
Akasema mwanangu nakupenda 
Usiitazame Leo yako mwanangu 
Ona mimi ni Mungu nikupendaye  .

Ni kweli kwa macho ya nyama Mimi nimechoka 
Wengi wanitazamapo kweli nimeshindwa 
Wengi wanionavyo kweli nimeshindwa 
Kweli kwa mbio za Mimi nimechoka 
Kweli kwa mwendo wangu nimeshindwa 
Kwa macho ya nyama nimechoka 
Kwa macho ya watu nimeshindwa 
Lakini hakuna hata mmoja 
Anayejua patano langu na Mungu
Lakini hakuna hata mmoja anayejua nimepatana nini 
Tumepatana na Baba hataniacha 
Hata nikisukwa sukwa sitamuacha 
Hata nikilia nisimuache 
Hata nikiteseka aah nisimwache 
Tumepatana na Baba 
Nimepatana na Baba 
Nimepatana na Baba 
Nimepatana na Baba  .

Naiona kesho yangu iliyonjema haa
Naiona kesho iliyonjema haa Mwenzenu 
Naionaaaa kesho  .

Naiona kesho kesho iliyopangwa na Baba (kesho ya heshima) 
Naiona kesho kesho iliyopangwa na Mungu (kesho ya Neema) 
Naiona kesho kesho iliyopangwa na Baba (kesho ya kufanikiwa) 
Kesho ya heshima aah, kesho ya utukufu iliyopangwa na Baba 
Kesho ya heshima (ya heshima yangu na mimi) 
iliyopangwa na Mungu (kesho ya wote kumjua Mungu wangu)
Kesho ya heshima iliyopangwa na Baba 
Kesho ya ushindi iliyopangwa na Mungu
Kesho ya utukufu wangu iliyopangwa na Baba 
Kesho, kesho, kesho .


Naiona Kesho Video

  • Song: Naiona Kesho
  • Artist(s): Martha Mwaipaja
  • Album: Naiona Kesho
  • Release Date: 14 May 2016
Naiona Kesho Audio Preview: Download / Stream : Amazon Music / iTunes


Share: