Martha Mwaipaja - Nifundishe Kunyamaza

Chorus / Description : Nifundishe kunyamaza
Nifundishe kunyamaza
Nisijejibu nikakukosea Mungu uu

Nifundishe Kunyamaza Lyrics

Nifundishe kunyamaza 
Nifundishe kunyamaza 
Nisijejibu nikakukosea Mungu uh
Nifundishe kunyamaza 
Nifundishe kunyamaza 
Nisijejibu nikakukosea Mungu uu

Weeh Baba wewe ni mwalimu mwema
We ewe Mungu wewe ni mwalimu mwema
Niko darasani kwako masia 
Baba naomba nifundishe kunyamaza
Niko katika kipindi hiki 
Bwana naomba nifundishe kunyamaza
Natamani kunyamaza ah 
Lakini si rahisi nifundishe kunyamaza
Natamani kunyamaza masia naomba nifundishe kunyamaza
Yapo mengi mambo yanayoweza fanya niseme
Yapo mazingira yanayoweza fanya nijibu nikakosea
Kwa maisha tunayoishi naomba nifundishe kunyamaza
Kwa ninayoyasikia kila siku Bwana nifundishe kunyamaza
Kwa ninayoyaona kila siku eh Baba nifundishe kunyamaza
Mmmh Wapo wanaoweza fanya nipambane eeh nipambane
Yapo yanayoweza fanya nishindane eeh nishindane
Bila neema ya kunyamaza naweza jikuta ninajibu vibaya
Bila neema ya kunyamaza naweza jikuta ninasema vibaya
Wee Yesu wewe naomba nifundishe kunyamaza
Wee Baba wewe naomba nifundishe kunyamaza 
Kwa macho nimeona mengi naomba nifundishe kunyamaza
Kwa vinywa nimenenewa mengi naomba nifundishe kunyamaza
Kwa masikio nimesikia mengi Bwana nifundishe kunyamaza 

Oh nifundishe kunyamaza 
nifundishe kunyamaza 
nisijejibu nikakukosea Mungu uu

Eeh Baba nisaidie Baba 
Ewe Mungu nisaidie Mungu
Ninatamana sana nijilinde nisije kukukosea
Ninachotaka nijilinde nisije kukupoteza
Watu wanaweza taka nipambane nikukose mwokozi 

Oh nifundishe kunyamaza 
Nifundishe kunyamaza 
Nisijejibu nikakukosea Mungu uu
Wengu wanataka nipambane nikukose mwokozi
...

Oh nifundishe kunyamaza 
nifundishe kunyamaza 
nisijejibu nikakukosea Mungu uu

Nifundishe Kunyamaza

  • Song: Nifundishe Kunyamaza
  • Artist(s): Martha Mwaipaja


Share: