Mercy Linah - Umenipa Uhai Baba

Chorus / Description : Kwa moyo wangu wote
Nasema ahsante Kwako
Messiah nashukuru
Baba nashukuru

Umenipa Uhai Baba Lyrics

Umenipa uhai Baba
Nafasi nyingine ya siku mpya, Baba nashukuru
Umeniponya roho na mwili
tabibu wa ajabu ewe Yesu, Baba nashukuru
Umeondoa laana Baba,
Kabadilisha kuwa baraka, Baba nashukuru
Kilio changu ewe Yesu Kabadilisha kuwa furaha
Baba nashukuru

Kwa moyo wangu wote
Nasema ahsante Kwako
Messiah nashukuru

Nilipokuwa mnyonge Baba
Umekuwa nguvu yangu,Baba nashukuru
Nayo mishale ya yule mwovu
Haijanipata Umenilinda, Baba nashukuru
Umeniongoza Mwokozi wangu
Kanisimamisha imara, Baba nashukuru
Umenitoa kwenye shimo la giza
kanileta kwenye mwanga, Baba nashukuru

Kwa moyo wangu wote
Nasema ahsante Kwako
Messiah nashukuru

Yale yote umetenda
Ni mengi mno na ya ajabu
Sijui mimi nisemeje?
Yale Yahweh Umenitendea
Ni mengi mno na ya ajabu
Sijui mimi nisemeje?
Sijui mimi nisemeje? eeh

Kwa moyo wangu wote
Nasema ahsante Kwako
Messiah nashukuru

Umenipa Uhai Baba Video

  • Song: Umenipa Uhai Baba
  • Artist(s): Mercy Linah


Share: