Chorus / Description :
Unapoomba omba kwa Imani maombi atayasikia,
unapoomba uwe mnyenyekevu, maombi atayajibu.
Unapoomba, nitaje Jina omba Mungu anikumbuke,
Ni mnyonge mimi sina uwezo, kwa maombi 'tapata nguvu.
Unapoomba omba kwa Imani maombi atayasikia,
unapoomba uwe mnyenyekevu, maombi atayajibu.
Kulala kwetu, kuamka kwetu, kuishi kwetu ni Neema,
tumaini letu li kwako Bwana, Abudu, ungama,
shukuru kwa dua zetu, tumaini letu li kwake Bwana.
Mungu ajibu maombi maombi ya watu wake.
Uliza, amini, pokea shukuru,
lingana ahadi zake ombi lako litajibiwa.