Chorus / Description :
Eeh Niko na ubaya, niko na ubaya
Niko na ubaya Bwana nibadilishe
Ooh Niko na ubaya, niko na ubaya
Niko na ubaya Bwana nibadilishe
Kwanza nimenyoa deni
Napenda sana mitindo ya nywele
Kuruka usiseme, viwanja vipya ninakaribisha
Kwenye kurasa za insta nakesha nikitafuta tena mabaya
Niki zigi napata nalitafuta tena nalipa wala silipi madeni
Nikikopa nabet wala sionangi ?
Fungu la kumi kwangu iyo ni story
Nasubiri jumapili ata unajua sina imani
Japo ninaitikia amini nasubiria ukitenda kwanza
Iyo nikubali,
Kama Yesu najua, na idadi ya vitabu najua
Na yalipo makanisa najua
Ila kuhudhuria nashindwa
Kwa ibada nasinzia sijui mdudu kaingia
Ila nikiona beer nasikia kuchangamka
Kwa ibada nasinzia sijui mdudu kaingia
Ila nikiona beer nasikia kuchangamka
Niko na ubaya, niko na ubaya
Niko na ubaya Bwana nibadilishe
Kuna vinyimbo vinanichoma hasa ile parapanda
Ikipigwa wakizikana pia sirudi kosa
Maneno yananichoma binadamu ni maua
Ikipita wiki moja masikini nasahau kabisa
Kwa ibada nasinzia sijui mdudu kaingia
Ila nikiona beer nasikia kuchangamka
Kwa ibada nasinzia sijui mdudu kaingia
Ila nikiona beer nasikia kuchangamka
Eeh Niko na ubaya, niko na ubaya
Niko na ubaya Bwana nibadilishe
Ooh Niko na ubaya, niko na ubaya
Niko na ubaya Bwana nibadilishe
Nakupa maisha na moyo utakase
Ninapoanguka nishike nisimame
Nakupa maisha na moyo utakase
Ninapoanguka nishike nisimame
Eeh Niko na ubaya, niko na ubaya
Niko na ubaya Bwana nibadilishe
Ooh Niko na ubaya, niko na ubaya
Niko na ubaya Bwana nibadilishe