Paul Clement - Amenifanyia Amani

Chorus / Description : Amenifanyia amani
Amenifanyia amani
Kaondoa huzuni yangu
Kanifanyia amani.

Amenifanyia Amani Lyrics

Amenifanyia amani
Amenifanyia amani
Kaondoa huzuni yangu
Kanifanyia amani.

Nijapopita, kwenye bonde la mauti
Sitaogopa, maana wewe uko nami
Gongo lako na fimbo yako, eh Bwana vyanifariji
Wanifanyia amani umesema, ya kwamba hutaniacha
Sababu mimi, ni mboni ya jicho lako
Bwana wanitazama, asubuhi, mchana, jioni
Eeh Bwana, kweli Mungu wa baraka

Amenifanyia amani
Amenifanyia amani
Kaondoa huzuni yangu
Kanifanyia amani.

Amebadilisha uchungu wangu, umekua ni furaha yangu
Oh huyu Yesu amenipa furaha
Kanifanyia amani
Amebadilisha machozi yangu yamekuwa ni furaha yangu oooh!
Huyu Yesu amenipa furaha kanifanyia amani

Amenifanyia amani
Amenifanyia amani
Kaondoa huzuni yangu
Kanifanyia amani.

Furaha unipayo siyo kama ya dunia hii
Amani unipayo siyo kama ya ulimwengu huu
Wewe waniganga moyo nipatapo uchungu
Wanifanyia amani

Amenifanyia furaha
Amenifanyia furaha
Kaondoa huzuni yangu
Kanifanyia furaha.

Amenifanyia Amani Video

  • Song: Amenifanyia Amani
  • Artist(s): Paul Clement


Share: