Chorus / Description :
Umeahidi wewe Bwana huniachi
Hadi mwisho wa dahari ulisema huniachi
Wewe ni Mungu uliye mwaminifu siku zote
Umeahidi wewe Bwana huniachi
Hadi mwisho wa dahari ulisema huniachi
Wewe ni Mungu uliye mwaminifu siku zote
Nipitiapo maji mengi au moto huniachi
Unalijua jina langu ewe bwana huniachi
Unatengeneza njia hata mito kule jangwani
Wewe ndiwe alpha na omega huniachi
Umeahidi wewe Bwana huniachi
Hadi mwisho wa dahari ulisema huniachi
Wewe ni Mungu uliye mwaminifu siku zote
Uliwalinda wana Israeli kule Jangwani
Ukamtoa danieli kutoka tundu la simba
Wewe huwainua na wanyonge siku zote
Watuepusha na hatari kila siku usifiwe
Umeahidi wewe Bwana huniachi
Hadi mwisho wa dahari ulisema huniachi
Wewe ni Mungu uliye mwaminifu siku zote
Marafiki nao wanaweza nigeuka
Mara kwa mara maadui wanizunguka
Nitaishi kwa ahadi yako bwana, huniachi huniachi
Umeahidi wewe Bwana huniachi
Hadi mwisho wa dahari ulisema huniachi
Wewe ni Mungu uliye mwaminifu siku zote