Chorus / Description :
Mbingu zahubiri utukufu wako Baba Mungu kweli eeh eh
Anga yatangaza kazi ya mikono yako Baba
Mchana husemezana na mchana
Na usiku hutolea usiku maarifa
Wewe umeumba vitu vyote na vya kupendeza Baba Mungu kweli
Mbingu zahubiri utukufu wako Baba Mungu kweli eeh eh
Anga yatangaza kazi ya mikono yako Baba
Mchana husemezana na mchana
Na usiku hutolea usiku maarifa
Wewe umeumba vitu vyote na vya kupendeza Baba Mungu kweli .
Maneno ya kinywa changu
Na mawazo ya moyo wangu
Yapate kibali mbele zako Bwana
Mwamba wangu mwokozi wangu .
Sheria yake Bwana ni kamilifu huiburudisha nafsi kweli
Ushuhuda wake Bwana ni amina humtia mjinga hekima
Maagizo yake Bwana ni adili huufurahisha moyo eeh eh
Amri yake Bwana ni safi safi mno huyatia macho nuru kweli .
Maneno ya kinywa changu
Na mawazo ya moyo wangu
Yapate kibali mbele zako Bwana
Mwamba wangu mwokozi wangu