Solomon Mukubwa - Umeniweza

Chorus / Description : Umeniweza Umeniweza
Umeniweza nimetulia

Umeniweza Lyrics

Umeniweza Umeniweza 
Umeniweza nimetulia 

Nilikuwa mbishi sana (umeniweza) 
Nilikuwa sisikii ooh (umeniweza) 
Umeniweza Bwana (umeniweza) 
Nimewezewa na wewe (umeniweza) 
(Nimetulia)

Mimi huyu hapa nilikuwa kam-very complicated sana 
Nilipokutana na wewe 
Nilikuwa kamubishi sana 
Nilikuwa napinga maneno yako Mungu 
Nilipokutana na wewe

Masikio yangu yalikuwa magumu nilikuwanga sisikiangi 
Yesu nilipokutana nawe (umeniweza nimetulia) 
Pombe nilikunywa sana bangi nilivuta sana 
Nilipokutana na wewe (umeniweza nimetulia) 

Umeniweza umeniweza Bwana 
Leo nimenyenyenyekea (umeniweza nimetulia) 
Leo nimetulia kwako 
Umenipa furaha ya wokovu Yesu 
Nilipotulia kwako Bwana 
Umenitengeneza mapito yangu 

Wengine wetu wamekunywa pombe mpaka wakalala mitaroni 
Walipokutana na wewe (umewaweza wametulia) 
Wengine walipata mshahara wakakimbilia geste na kahaba 
Walipokutana na wewe (umewaweza wametulia) 
Wengine walikuwa ni waasi wa neno lako 
Walipokutana na wewe (umewaweza wametulia) 
Wengine walikuwa na michanuko walipokutana na Yesu 
michupuko imeanguka chini 
Walipokutana na wewe (umewaweza wametulia) 
Wengine walikuwa na mipango ya kando 
Walipokutana na Yesu mipango ya kando imeanguka 
(umewaweza wametulia)  

Mwanaume Yesu wee Yesu umetuweza 
(umeniweza nimetulia) 
Nimesaluti kwako (umeniweza) 
Yesu umetuweza (umeniweza) 
(umeniweza nimetulia) 

Waliokuwa wahuni wamekugeukia (umeniweza) 
Umewaweza Yesu wamerudi kwa maisha 
(umeniweza nimetulia)

Umeniweza eeeh, umeniweza Baba (umeniweza) 
Umeniweza nashindwa kuongea (umeniweza nimetulia) 

Ameniweza ameniweza (umeniweza) 
...

Umeniweza Video

  • Song: Umeniweza
  • Artist(s): Solomon Mukubwa


Share: