Emachichi - Liko Lango Moja Wazi - Lango ndiye yesu Bwana

Chorus / Description : Liko lango moja wazi, ni lango la mbinguni;
Na wote waingiao watapata nafasi.
Yesu ndiye lango hili, hata sasa ni wazi,
Kwa wakubwa na wadogo, tajiri na maskini.

Liko Lango Moja Wazi - Lango ndiye yesu Bwana Lyrics

Liko lango moja wazi, ni lango la mbinguni;
Na wote waingiao watapata nafasi.

Yesu ndiye lango hili, hata sasa ni wazi,
Kwa wakubwa na wadogo, tajiri na maskini.

Hili ni lango la raha,ni lango la rehema;
Kila mtu apitaye hana majonzi tena.

Tukipita lango hili tutatua mizigo,
tuliochukua kwanza, tutavikwa uzima.
Liko Lango Moja Wazi - Lango ndiye yesu Bwana Video

  • Song: Liko Lango Moja Wazi - Lango ndiye yesu Bwana
  • Artist(s): Emachichi


Share: