Chorus / Description :
nitamjua, nikimwona uso kwa uso;
nitamjua kwa alama za misumari
Kazi yangu ikiisha, nami nikiokoka
Kazi yangu ikiisha, nami nikiokoka
Na kuvaa kutokuharibika, Nitamjua Mwokozi nifikapo ng?amboni
Atakuwa wa kwanza kunilaki.
Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.
Furaha nitapata nikiona makao Bwana aliyotuandalia;
Nitamsifu mwokozi kwa rehema na pendo
Vilivyonipa pahali Mbinguni.
Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.
Nao waliokufa katika Bwana Yesu, Nitawaona tena huko juu;
Lakini nifikapo kwake huko Mbinguni, Nataka kumwona Mwokozi kwanza.
Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.
Milangoni mwa mji Bwana atanipitisha,
Pasipo machozi wala huzuni.
Nitauimba wimbo wa milele;
lakini Nataka kumwona Mwokozi kwanza.
Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.
# I will Know Him