The Saints Ministers - Mifulizo Ya Baraka

Chorus / Description : Twala, twanywa, twalala, twaamka,
uaminifu wako kwetu mkuu,
Hitaji letu tunalo
baraka zako zafululiza twashukuru kwazo.

Mifulizo Ya Baraka Lyrics

Mungu, Elshadai wetu, matendo yako makuu, 
umetukamilisha twajivunia (mifulizo) ya baraka zako.

Twala, twanywa, twalala, twaamka, 
uaminifu wako kwetu mkuu, 
Hitaji letu tunalo 
baraka zako zafululiza twashukuru kwazo.

1. Hannah alibezwa kwa kukosa mtoto, 
hakukataa tamaa, aliomba, wakati wa Mungu ulipofika 
Samweli kazaliwa baraka nyumbani mwake.

2. Waangalieni Ndege wa angani, hawapandi wala hawavuni, 
hawakusanyi ghalani, ila Baba wa mbinguni huwalisha hao.

Twala, twanywa, twalala, twaamka, uaminifu wako kwetu mkuu, 
Hitaji letu tunalo baraka zako zafululiza twashukuru kwazo.

Wengine walala hoi nawe wala na kusaaza wahitaji nini? 
Mbona walilia cheo wengine hawana kazi, wahitaji nini? 
Wengine wamelazwa na wewe una afya.. Mshukuru Mungu..

Hesabu mibaraka moja moja, aogeleavyo papa baharini,  
Mwanga wa jua hung'aa kote mvua ya masika hutunyea ilivyo baraka zake. 

Ilivyo nyota angani ndivyo baraka zake, Utukuzwe Mungu. 

Mungu, Elshadai wetu, matendo yako makuu, 
umetukamilisha twajivunia (mifulizo) ya baraka

Mifulizo Ya Baraka Video

  • Song: Mifulizo Ya Baraka
  • Artist(s): The Saints Ministers


Share: