Chorus / Description :
Mimi nikae miguuni pako
Ninaomba Baba unifundishe
Roho wa Mungu mwalimu mwema
Ninaomba Baba unifundishe
Eh Bwana Yesu niko mbele zako Baba
Ninakuomba Baba unisikie
Nahitaji nikujue niyajue maneno yako
Yesu sheria zako Mungu zikae ndani yangu
Uliwaambia waisraeli wazishike sheria zako Bwana
Kusudi baraka zako ziwe juu yao
Unishike nisipotee nikaenda kwa njia isiyofaa
Nikaliacha neno nikapotea
Unilinde mguu wangu nisiuate mabaya
Adui asinimeze nikaangamia
Huduma yangu mimi utumishi wangu mimi
Popote ninapohudumu nikusifu Yesu
Kote ulikonitoa mengi umenitendea mimi
Nisije nikasahau wema wako Mungu
Mimi nikae miguuni pako
Ninaomba Baba unifundishe
Roho wa Mungu mwalimu mwema
Ninaomba Baba unifundishe
Utusamehe watumishi mara nyingi tumekukosea Baba
Tunavyojiinua na tunakusahau
Miujizi ikitendeka tunasema ni kwa nguvu zako wewe
Tunasahau kwamba wewe umetenda
Tunatumia madhabau kuyakuza majina yetu sisi
Badala ya kulikuza jina lako Yesu
Tumesahau mapatano tulikuahidi ukituinua Baba
Tutakuinua Yesu mataifa wakujue
Hata sisi watumishi tumeshindwa kuzifuata amri zako
Tunatamani sana kulirekebisha neno
Na kama ungeturusu tuweze kulirekebisha neno
Kila mtu angejiongoza anavyotaka yeye
Tunafanya mazingaombwe kwenye madhabau Yesu
Tunadhani tunaweza kusaidia Mungu
Lakini mimi nikae miguuni pako
Ninaomba Baba unifundishe
Roho wa Mungu mwalimu mwema
Ninaomba Baba unifundishe