Upendo Nkone - Usifurahi Juu Yangu eeh Adui

Chorus / Description : Usifurahi juu yangu eeeh adui yangu,
niangukapo mimi nitasimama tena.
Kumbuka niwapo gizani bwana nuru yangu,
hawezi kuniacha bwana mimi niangamie.
Ujue kwa maombi yako mimi nitasimama tena,
Ujue kwa maombi yako nitabarikiwa,
Ujue kwa maombi yako mimi nitasimama tena,
Ujue kwa maombi yako nitabarikiwa,

Usifurahi Juu Yangu eeh Adui Lyrics

Usifurahi juu yangu eeeh adui yangu,
niangukapo mimi nitasimama tena.
Kumbuka niwapo gizani bwana nuru yangu,
hawezi kuniacha bwana mimi niangamie.

Si vyema kunisema vibaya nipatapo tatizo,
shetani wampa nafasi ndani ya moyo wako
Kumbuka kwa maombi yako nitasimama tena,
na utapata baraka kutoka kwake Mungu

Maana heri mtu yule ambaye kinywa chake,
huwabariki wenzake na kuwaombea.
Maana maneno mabaya huuchafua moyo.
kukuweka mbali na Mungu ni vema uwe safi.

Ukiona nipo kwenye shida (niombee),
Ndoa yangu imevunjika wewe niombee,
Nikifukuzwa kazini ndugu niombee,
Magonjwa yananiandama niombee,
Biashara haina faida niombee,
Nikikawia kupata mtoto nimbee,
Nimekuwa mtoto yatima niombee,
Hata nijapokuwa mjane niombee,

Ujue kwa maombi yako mimi nitasimama tena,
Ujue kwa maombi yako nitabarikiwa,
Ujue kwa maombi yako mimi nitasimama tena,
Ujue kwa maombi yako nitabarikiwa,

Usifurahi Juu Yangu

  • Song: Usifurahi Juu Yangu eeh Adui
  • Artist(s): Upendo Nkone


Share: