Martha Mwaipaja - Mambo Yamebadilika

Chorus / Description : Mambo yamebadilika, mambo yamebadilika
Ukieleza mambo yangu eleza ya sasa

Mambo Yamebadilika Lyrics

Mambo yamebadilika, mambo yamebadilika 
Ukieleza mambo yangu eleza ya sasa 
Mambo yangu si vile, neema ameniona 
Mambo yamebadilika eleza ya leo

Mambo yamebadilika, mambo yamebadilika 
Ukieleza mambo yangu eleza ya sasa 

Haa, wewe ni kila kitu Yesu 
Naa naa naah nimetamwa na mimi 
Mungu amenitoa mbali na mimi 
Wakati kuzimu ilipanga kila siku nilie 
Hivyo mbingu ilipanga nami nifurahi 
 
Nilipochimbiwa shimoni nizame nisitoke tena 
Hivyo mbingu ilipanga nitatoka namna gani 
Ni vile hukujua ninapendwa na Mungu 
Hukutambua nami nimefarijiwa 
Ulieleza mabaya kila ulipopita 
Naomba na leo tangaza haya mema 
Waambie watu Mungu si mwanadamu 
Mwambie watu amejawa na huruma 
Mwambie Mungu ni wa wote kweli 
Hana upendeleo kabisa 
Usiwaambie watu mambo mabaya mabaya 
Jifunze kusema yaliyo mema

Mambo yamebadilika, mambo yamebadilika 
Ukieleza mambo yangu eleza ya sasa 

Usiwaambie watu yule ni masikini 
Waambie sasa amebarikiwa 
Usiwaambie watu ule ni mama mjane tu 
Waambie Yesu ni mume wa wajane 
Usiwaambie ule ni mtoto yatima tu 
Waambie Mungu ni Baba wa yatima 
Usiwaambie watu yule ni mgonjwa namjua 
Waambie Mungu anaponya kila kitu... 

Mambo yamebadilika, mambo yamebadilika 
Ukieleza mambo yangu eleza ya sasa 


Mambo Yamebadilika Video

  • Song: Mambo Yamebadilika
  • Artist(s): Martha Mwaipaja
  • Album: Mambo Yamebadilika - Single
  • Release Date: 28 Dec 2020
Mambo Yamebadilika Audio Preview: Download / Stream : Amazon Music / iTunes


Share: