Mercy Linah - Huniongoza

Chorus / Description : Huongoza hunishika, kwa mkono wa hakika
Nitaandamana naye Kristo aniongozaye

Huniongoza Lyrics

Huniongoza Mwokozi,
ndipo nami hufurahi
Niendapo pote napo,
ataniongoza papo

Huongoza hunishika, kwa mkono wa hakika
Nitaandamana naye Kristo aniongozaye

Pengine ni mashakani,
nami pengine rahani
Ni radhi ijayo yote,
yupo nami siku zote

Huongoza hunishika, kwa mkono wa hakika
Nitaandamana naye Kristo aniongozaye

Mkono akinishika,
kamwe sitanung?unika
Atachoniletea,
ni tayari kupokea

Huongoza, hunishika kwa mkono wa hakika
Nitaandamana naye Kristu aniongozaye

Nikiishika kazi chini,
nitakwenda huko mbinguni
Nako nitamtukuza,
Kristo aliyeniongoza

Huongoza hunishika, kwa mkono wa hakika
Nitaandamana naye Kristo aniongozaye

Nitaandamana naye kristo aniongozaye 
Nitaandamana naye kristo aniongozaye
Nitaandamana naye kristo aniongozaye

Huniongoza Video

  • Song: Huniongoza
  • Artist(s): Mercy Linah


Share: