Reuben Kigame - Mbingu Zahubiri

Chorus / Description : Mbingu zahubiri utukufu wako Baba Mungu kweli eeh eh
Anga yatangaza kazi ya mikono yako Baba
Mchana husemezana na mchana
Na usiku hutolea usiku maarifa
Wewe umeumba vitu vyote na vya kupendeza Baba Mungu kweli

Mbingu Zahubiri Lyrics

Mbingu zahubiri utukufu wako Baba Mungu kweli eeh eh 
Anga yatangaza kazi ya mikono yako Baba 
Mchana husemezana na mchana 
Na usiku hutolea usiku maarifa 
Wewe umeumba vitu vyote na vya kupendeza Baba Mungu kweli  .

Maneno ya kinywa changu 
Na mawazo ya moyo wangu 
Yapate kibali mbele zako Bwana 
Mwamba wangu mwokozi wangu  .

Sheria yake Bwana ni kamilifu huiburudisha nafsi kweli 
Ushuhuda wake Bwana ni amina humtia mjinga hekima 
Maagizo yake Bwana ni adili huufurahisha moyo eeh eh 
Amri yake Bwana ni safi safi mno huyatia macho nuru kweli  .

Maneno ya kinywa changu 
Na mawazo ya moyo wangu 
Yapate kibali mbele zako Bwana 
Mwamba wangu mwokozi wangu 

Mbingu Zahubiri Video

  • Song: Mbingu Zahubiri
  • Artist(s): Reuben Kigame + Sifa Voices


Share: