Sifa Music - 46 Twae Wangu Uzima

Chorus / Description : Take my life and let it be Swahili hymn
Twae wangu uzima,
Sadaka ya daima;
Twae saa na siku,
Zikutukuze huku.

46 Twae Wangu Uzima Lyrics

Twae wangu uzima,
Sadaka ya daima;
Twae saa na siku,
Zikutukuze huku.

Twae mikono nayo
Ifanye upendavyo,
Twae yangu miguu
Kwa wongozi wako tu.

Twae sauti yangu,
Niimbe kwa Mungu tu;
Itwae na midomo,
Ijae neno lako.

Twae dhanabu pia,
Na yote ya dunia;
Twae yangu hekima,
Upendavyo tumia.

Nia itwae, Mungu,
Haitakuwa yangu;
Twae moyo; ni wako,
Uwe makazi yako.

Twae mapenzi yangu,
Sifa za moyo wangu;
Twae kabisa nafsi
Nniwe wako halisi.

46 Twae Wangu Uzima Video

  • Song: 46 Twae Wangu Uzima
  • Artist(s): Sifa Music


Share: