Msifuni Yesu Ndiye Mkombozi Lyrics + Video

Swahili Songs Playlist Music Videos

Msifuni Yesu Ndiye Mkombozi Lyrics

Mp3 Song

Msifuni ,Yesu ndiye mkombozi; Imbeni ya pendo zake kuu,
Sujuduni,malaika mlioko, Jina lake liwe na sifa kuu.
Kama vile mchunga uchungavyo Vivyo sisi kutwa atachunga.
Msifuni mlio wake watoto Msifuni aliye mchunga.

Msifuni,Yesu ndiye mkombozi; Akateswa tupate ongoka;
Ndiye Mwamba,Dhamana ya kuokoka;
Sujuduni kwake muangikwa, Yesu aliyeudhiwa na hamu Kwa pendo za baba yake Mungu. Aliyefyolewa na kusulubiwa. Msifuni ndilo letu fungu.

Msifuni,Yesu ndiye Mkombozi; Shindukeni,enyi malango juu;
Bwana Yesu tangu milele Mwokozi, Mvikeni taji, ni yake tu.
Atakuja kuitawala nchi, Yesu,Mwombezi wetu wa Mungu.
Msifuni, ni mfalme wa salama; Ndiye kweli mwana wake Mungu.Top Songs United States
Share:

Write a review/comment/correct the lyrics of Msifuni Yesu Ndiye Mkombozi:

0 Comments/Reviews