Emachichi - kazi yangu ikiisha nami nikiokoka - Nitamjua

Chorus / Description : nitamjua, nikimwona uso kwa uso;
nitamjua kwa alama za misumari
Kazi yangu ikiisha, nami nikiokoka

kazi yangu ikiisha nami nikiokoka - Nitamjua Lyrics

Kazi yangu ikiisha, nami nikiokoka
Na kuvaa kutokuharibika, Nitamjua Mwokozi nifikapo ng?amboni
Atakuwa wa kwanza kunilaki.

Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.

Furaha nitapata nikiona makao Bwana aliyotuandalia;
Nitamsifu mwokozi kwa rehema na pendo
Vilivyonipa pahali Mbinguni.

Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.

Nao waliokufa katika Bwana Yesu, Nitawaona tena huko juu;
Lakini nifikapo kwake huko Mbinguni, Nataka kumwona Mwokozi kwanza.

Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.

Milangoni mwa mji Bwana atanipitisha,
Pasipo machozi wala huzuni.
Nitauimba wimbo wa milele;
lakini Nataka kumwona Mwokozi kwanza.

Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.

# I will Know Him

kazi yangu ikiisha nami nikiokoka - Nitamjua Video

  • Song: kazi yangu ikiisha nami nikiokoka - Nitamjua
  • Artist(s): Emachichi

Share: