Danieli Mlango 1 Daniel

Danieli 1:1 Daniel 1:1

Katika mwaka wa tatu wa kumiliki kwake Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, Nebukadreza mfalme wa Babeli,alikwenda Yerusalemu akauhusuru.

Danieli 1:2 Daniel 1:2

Bwana akamtia Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, katika mkono wake, pamoja na baadhi ya vyombo vya nyumba ya Mungu; naye akavichukua mpaka nchi ya Shinari, mpaka nyumba ya mungu wake; akaviingiza vile vyombo katika nyumba ya hazina ya mungu wake.

Danieli 1:3 Daniel 1:3

Mfalme akamwambia Ashpenazi, mkuu wa matowashi wake, awalete baadhi ya wana wa Israeli, wa uzao wa kifalme, na wa uzao wa kiungwana;

Danieli 1:4 Daniel 1:4

vijana wasio na mawaa, wazuri wa uso, wajuzi wa hekima, werevu kwa sababu ya maarifa yao, wenye kufahamu elimu, watakaoweza kusimama katika jumba la mfalme; tena alimwambia awafundishe elimu ya Wakaldayo, na lugha yao.

Danieli 1:5 Daniel 1:5

Huyo mfalme akawaagizia posho ya chakula cha mfalme, na ya divai aliyokunywa, akaagiza walishwe hivyo muda wa miaka mitatu; ili kwamba hatimaye wasimame mbele ya mfalme.

Danieli 1:6 Daniel 1:6

Basi katika hao walikuwapo baadhi ya wana wa Yuda, Danielii, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria.

Danieli 1:7 Daniel 1:7

Mkuu wa matowashi akawapa majina; alimwita Danielii, Belteshaza; na Hanania akamwita Shadraka; na Mishaeli akamwita Meshaki; na Azaria akamwita Abednego.

Danieli 1:8 Daniel 1:8

Lakini Danielii aliazimu moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme, wala kwa divai aliyokunywa; basi akamwomba yule mkuu wa matowashi ampe ruhusa asijitie unajisi.

Danieli 1:9 Daniel 1:9

Basi Mungu alimjalia Danielii kupata kibali na huruma machoni pa huyo mkuu wa matowashi.

Danieli 1:10 Daniel 1:10

Mkuu wa matowashi akamwambia Danielii, Mimi namwogopa bwana wangu, mfalme, aliyewaagizia ninyi chakula chenu na kinywaji chenu; kwa nini azione nyuso zenu kuwa hazipendezi kama nyuso za vijana hirimu zenu? Basi kwa kufanya hivyo mtahatirisha kichwa changu mbele ya mfalme.

Danieli 1:11 Daniel 1:11

Ndipo Danielii akamwambia yule msimamizi, ambaye mkuu wa matowashi amemweka juu ya Danielii, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria,

Danieli 1:12 Daniel 1:12

Tafadhali utujaribu sisi watumishi wako muda wa siku kumi; na watupe mtama tule, na maji tunywe.

Danieli 1:13 Daniel 1:13

Kisha nyuso zetu zitazamwe mbele yako, na nyuso za wale vijana wanaokula chakula cha mfalme; ukatutendee sisi watumishi wako kadiri ya utakavyoona.

Danieli 1:14 Daniel 1:14

Basi akawasikiliza katika jambo hilo, akawajaribu siku kumi.

Danieli 1:15 Daniel 1:15

Hata mwisho wa zile siku kumi nyuso zao zilikuwa nzuri zaidi, na miili yao ilikuwa imenenepa zaidi, kuliko wale vijana wote waliokula chakula cha mfalme.

Danieli 1:16 Daniel 1:16

Basi yule msimamizi akaiondoa posho yao ya chakula, na ile divai waliyopewa wanywe, akawapa mtama tu.

Danieli 1:17 Daniel 1:17

Basi, kwa habari za hao vijana wanne, Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima; Danielii naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto.

Danieli 1:18 Daniel 1:18

Hata mwisho wa siku zile alizoziagiza mfalme za kuwaingiza, mkuu wa matowashi akawaingiza mbele ya mfalme Nebukadreza.

Danieli 1:19 Daniel 1:19

Naye mfalme akazungumza nao; na miongoni mwao wote hawakuonekana waliokuwa kama Danielii, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria; kwa hiyo wakasimama mbele ya mfalme.

Danieli 1:20 Daniel 1:20

Na katika kila jambo la hekima na ufahamu alilowauliza mfalme, akawaona kuwa walifaa mara kumi zaidi ya waganga na wachawi waliokuwa katika ufalme wake.

Danieli 1:21 Daniel 1:21

Tena, Danielii huyo akadumu huko hata mwaka wa kwanza wa mfalme Koreshi.