Angela Chibalonza - 29 Baba yetu aliye Mbinguni - Anipenda Mwokozi Yesu

Chorus / Description : I am so glad that our father in heaven swahili hymn
Anipenda Mwokozi Yesu, anipenda, anipenda;
Anipenda Mwokozi Yesu, anipenda mimi.

29 Baba yetu aliye Mbinguni - Anipenda Mwokozi Yesu Lyrics

Baba yetu aliye mbinguni, amenifurahisha yakini,
kuniambia mwake chuoni, ya kuwa nami Yesu pendoni.

Anipenda Mwokozi Yesu, anipenda, anipenda;
Anipenda Mwokozi Yesu, anipenda mimi.

Nimuachapo kutanga mbali, yeye yu vivyo, hupenda kweli,
hunirejeza kwake moyoni; kweli yu nami Yesu pendoni.

Anipenda! Nami nampenda; kwa wokovu alionitenda;
akanifia Msalabani, kwa kuwa nami Yesu pendoni.

Haya kujua yanipa raha; kumuamini kuna furaha;
Humfukuza mara shetani, kwona yu nami Yesu Pendoni.

Sifa ni nyingi asifiwazo, moja ni sana katika hizo,
wala siachi, hata Mbinguni, kwimba, "Yu nami Yesu pendoni".

  • Song: 29 Baba yetu aliye Mbinguni - Anipenda Mwokozi Yesu
  • Artist(s): Angela Chibalonza


Share: