Msalaba ndio asili ya mema Lyrics

Sioni haya kwa Bwana,
Kwake nitang’ara!
Mti wake sitakana,
Ni neno imara.

(Chorus)
Msalaba ndio asili ya mema,
Nikatua mzigo hapo;
Nina uzima, furaha daima,
Njoni kafurahini papo.

Kama kiti chake vivyo,
Ni yake ahadi;
Alivyowekewa navyo,
Kamwe, havirudi.

Bwana wangu, tena Mungu,
Ndilo lake jina!
Hataacha roho yangu,
Wala kunikana.

Atakiri langu jina,
Mbele za Babaye,
Anipe pahali tena,
Mbinguni nikae

# At the Cross


Msalaba ndio asili ya mema Video


Msalaba Ndio Asili Ya Mema - ( Tenzi Za Roho )


MSALABA NDIO ASILI YA WEMA (WORSHIP BY PATRICK MBARIA)


Msalaba Ndio Asili Angela Chibalonza Sioni Haya

Angela Chibalonza Sioni Haya Official Video


At The Cross Swahili

Mtunga Maneno: Isack Watts (1674-1748)
Mtunga Sauti: R. E. Hudson
Kiingereza: At the CrossShare:

Write a review/comment/correct the lyrics of Msalaba Ndio Asili Ya Mema:

1 Comments/Reviews

  • OBRIGHT BLESSED

    I love the song as a whole,it has strong teaching."For sure there is power on the cross,that unburdens every burden of Human kind