Christ Ambassadors - Moyoni Mwangu

Chorus / Description : Moyoni mwangu ninashukuru jina lake Bwana
Na roho yangu inafurahi kwa sababu ya pendo lake

Mungu wangu Bwana Wangu Ulipenda ulimwengu
Ukamtuma mwana wako aje atukomboe
Nasi tunakushukuru sababu ya pendo lako

Moyoni Mwangu Lyrics

Moyoni mwangu ninashukuru jina lake Bwana
Na roho yangu inafurahi kwa sababu ya pendo lake
Alitupenda sisi wandamu ooh alitupenda
Akamtuma Yesu mwanawe aje atuokoe

Ooh Mungu Wangu
Mungu wangu Bwana Wangu, Ulipenda ulimwengu
Ukamtuma mwana wako, aje atukomboe
Nasi tunakushukuru sababu ya pendo lako x2

Tangu sasa watu wa dunia wamshukuru Mungu
Ametimiza ahadi yake kweli ametupendeza
Pendo lake halina kipimo ooh alitupenda
Bila shaka ametuokoa tumwimbie kwa Shangwe

Mungu wangu Bwana Wangu, Ulipenda ulimwengu
Ukamtuma mwana wako, azeje atukomboe
Nasi tunakushukuru sababu ya pendo lako

Mungu wangu Bwana Wangu, Ulipenda ulimwengu
Ukamtuma mwana wako, azeje atukomboe
Nasi tunakushukuru sababu ya pendo lako





Moyoni Mwangu Video

  • Song: Moyoni Mwangu
  • Artist(s): Christ Ambassadors


Share: