Chorus / Description :
Kwetu pazuri nimeshapakumbuka
Ninayo hamu kuishi na mwokozi wangu
Kwa amani na furaha tena ya ajabu
Sipati picha kwa watakaofika
kwetu mbinguni
Ninayo hamu kurudi nyumbani
Nyumbani kwetu ambapo hatutatengana
Hapo nyumbani kwetu hakuna makaburi
Wala hakuna vyandarua maana hakuna malaria
Kwetu ni pazuri ni pazuri nakuambia
Najua nawe ndugu yangu unayo hamu ya kufika huko
Kwetu pazuri nimeshapakumbuka
Ninayo hamu kuishi na mwokozi wangu
Kwa amani na furaha tena ya ajabu
Sipati picha kwa watakaofika
kwetu mbinguni
Hii dunia imejaa shida
Kama hujui nenda hospitali kaone
Lakini kwetu hakuna fani ya tabibu
Watakatifu watachuma
Majani ya mti wa uzima wawe na afya
Hawataugua magonjwa tabu
Tutaziacha zote hapa duniani
Kwetu pazuri nimeshapakumbuka
Ninayo hamu kuishi na mwokozi wangu
Kwa amani na furaha tena ya ajabu
Sipati picha kwa watakaofika
kwetu mbinguni
Mpendwa njoo turudi nyumbani
Asubuhi yaja tuyakimbie ya dunia
Atakayekosa hapo kweli ni hasara
Aya matatizo ni mitego ya shetani
Ili tushindwe kufika nyumbani
Kwetu pazuri
Lakini kwa jina jina la yesu
Tumemshinda tunaenda
Kwetu pazuri nimeshapakumbuka
Ninayo hamu kuishi na mwokozi wangu
Kwa amani na furaha tena ya ajabu
Sipati picha kwa watakaofika
kwetu mbinguni