Chorus / Description :
Nimekupata yesu, nimepata yote,
Nimekupata bwana, sitahitaji tena aah,
Natamani nitembee katika upendo wa bwana,
Upendo ule wa dhati, upendo husiobagua,
Upendo uletao hekima, busara na amani,
Upendo wakimbingu pekee ulio bora
Nimekupata yesu, nimepata yote,
Nimekupata bwana, sitahitaji tena aah,
Wewe ndiwe hitaji langu,
Ngome yangu na mwamba
tengemeo langu katika hali
jaza moyo wangu, upendo nikupende,
U rafiki wa kweli, nifundishe kupenda aah,bwana,
maana upendo wako, ndio pekee waweza,
Kunifanya kiumbe kipya nikakufuate
Natamani nitembee katika upendo wa bwana,
Upendo ule wa dhati, upendo husiobagua,
Upendo uletao hekima, busara na amani,
Upendo wakimbingu pekee ulio bora
Wapenzi wa kulia, wengi ni wadanganyifu,
niwapo katika hali zuri tuko wote eeh,
lakini katika matatizo, wote wanikimbia,
wewe nimekupata nitakushikilia
Natamani nitembee katika upendo wa bwana,
Upendo ule wa dhati, upendo husiobagua,
Upendo uletao hekima, busara na amani,
Upendo wakimbingu pekee ulio bora
Nakukaribisha bwana, uyatawale maisha, yetu ya kila siku,
Tufundishe kupanda aah, mbegu Za upendo wa dhati,
mwisho wa nyakati,tuweze kuvuna matunda ya ukamili
kamilisha upendo, mungu aliohadaa
Dumisha ndoa zao furaha itawale,
Bwana, pembeni za unyonge na udhaifu wao
familia iwe mwanga wa mbingu ku
Natamani nitembee katika upendo wa bwana,
upendo ule wa dhati, upendo husiobagua,
upendo uletao hekima, busara na amani,
upendo wakimbingu pekee ulio bora