Chorus / Description :
Moyoni mwangu ninashukuru jina lake Bwana
Na roho yangu inafurahi kwa sababu ya pendo lake
Mungu wangu Bwana Wangu Ulipenda ulimwengu
Ukamtuma mwana wako aje atukomboe
Nasi tunakushukuru sababu ya pendo lako
Moyoni mwangu ninashukuru jina lake Bwana
Na roho yangu inafurahi kwa sababu ya pendo lake
Alitupenda sisi wandamu ooh alitupenda
Akamtuma Yesu mwanawe aje atuokoe
Ooh Mungu Wangu
Mungu wangu Bwana Wangu, Ulipenda ulimwengu
Ukamtuma mwana wako, aje atukomboe
Nasi tunakushukuru sababu ya pendo lako x2
Tangu sasa watu wa dunia wamshukuru Mungu
Ametimiza ahadi yake kweli ametupendeza
Pendo lake halina kipimo ooh alitupenda
Bila shaka ametuokoa tumwimbie kwa Shangwe
Mungu wangu Bwana Wangu, Ulipenda ulimwengu
Ukamtuma mwana wako, azeje atukomboe
Nasi tunakushukuru sababu ya pendo lako
Mungu wangu Bwana Wangu, Ulipenda ulimwengu
Ukamtuma mwana wako, azeje atukomboe
Nasi tunakushukuru sababu ya pendo lako