SAFARI BADO Lyrics

Mfalme Belshazzar maandiko yanamsimulia
Alilewa madaraka akamkosea Mungu
Alipopata ufalme alichanganyikiwa
Mpaka akathubutu kutumia vikombe vya hekalu.
Mfalme Belshazzar
Alishangaa kuona mkono unaandika ukutani
Na anayeandika alikuwa haonekani

Maneno yaliyo jitokeza ukutani yalikuwa haya
Mene Mene Tekeli na Peresin
Maana yake ufalme wako umepimwa kwa mizani
Nao umeonekana umepungua
Ufalme wako wamegawanywa wabedi na wajemi Belshazzar Belshazzar
Belshazzar alidhani amefika akaanza kudharau watu kumbe safari bado
Mfalme Belshazzar alidhani amefika, akaanza kumdharau Mungu kumbe safari bado Inaendelea
Safari bado, Maisha ni s safari baaado.safari bado... inaendelea

Bado safari bado, Bado
Maisha ni safari ndefu ndungu safari bado
Bado safari bado Ndugu yangu
Usianze kudharau watu ndugu safari bado
Bado safari bado
Endelea kumheshimu Mungu ndungu safari bado inaeendelea, safari bado


Ukipigiwa simu haupokei unaiangalia tu
Unadhani umefika kumbe safari bado
Ukipita na gari yako matope unaturushia
Unadhani umefika kumbe safari bado
Umejifungua salama usifute namba za wakunga
Ndugu yangu nakukumbusha kwamba safari bado
Bado safari baaado
Endelea kuheshimu watu ndungu safari bado
Baadoo safari baaado
Usiache kumwabudu Mungu ndugu safari bado. inaeendelea


Bado safari bado, Bado
Maisha ni safari ndefu ndungu safari bado
Bado safari bado Ndugu yangu
Usianze kudharau watu ndugu safari bado
Bado safari bado
Endelea kumheshimu Mungu ndungu safari bado inaeendelea, safari bado.

Umesoma sawa lakini kumbuka walio kusomesha
Usiwasahau maana safari bado
Una pesa nyingi sawa lakini kumbuka ulikotoka
Usidharau watu ndungu safari bado
Bado safari bado
Endelea kuheshimu watu ndungu safari bado
Bado safari bado
Maisha ni safari ndefu ndungu safari bado Inaendelea
Safari bado heiyee

Bado safari bado, Bado
Maisha ni safari ndefu ndungu safari bado
Bado safari bado Ndugu yangu
Usianze kudharau watu ndugu safari bado
Bado safari bado
Endelea kumheshimu Mungu ndungu safari bado inaeendelea, safari bado

@ Bonny Mwaitage Featuring Bahati Bukuku

SAFARI BADO VideoShare:

Write a review/comment/correct the lyrics of Safari Bado:

0 Comments/Reviews