Soma Mwanangu Lyrics

Mshike sana elimu usimwache aende zake,
ni maneno ya mungu kutoka kwenye vitabu vitakatifu ,
mimi enzi zangu maneno hayo si kuyajua,
nilifanya mchezo sikuweka uzito kwenye elimu ,
hivyo, nilishindwa kusoma,
ndio maana namuomba mungu mtoto wangu usome ,
hivyo mimi baba yako nilishindwa kusoma ,
ndio maana namuomba mungu mtoto wangu usome,
soma

Baba yako anapenda ,mwanangu usome,
Mama yako anapenda ,mwanangu usome

Namuomba mungu akusaidie sana mwanangu usome
Namuomba mungu akupiganie wewe mwanangu usome

Usifanye mchezo ukiwa darasani mwanangu,
mimi na mama yako tunapenda sana usome ,
ukifanya mchezo maisha yetu mwenyewe unayajua,
ukifanya mchezo tutakuwa wageni wa nani,
Soma ,soma mwanangu,
soma we,soma mwanangu pengine,
utakuja kutuokoa we,baadaye

Mimi baba yako sikubahatika kusoma ,
soma mwana, usome wewe,
pengine unaweza okoa familia yetu
Kazi ya ulinzi ni ngumu nakulilia we usoma,
soma we mwanangu
(mama yako pia anapenda usome)
Nabeba kirungu nang'atwa na mbu usiku kucha,
kwa ajili yako mwanangu,soma we
(Mama yako anapenda, Mwanangu soma)
Maisha bila elimu ni magumu, soma we
Mimi na mama yako hatuchoki kukuombea Mungu akusaidie
Nimebeba zege pesa yote nimepeleka shule, soma
Robo tatu ya mshahara wangu wote nimepeleka shule
(Mama yako anapenda, Mwanangu soma)
Tumeuza ng'ombe pesa zote tumepeleka shule
(Mama yako anapenda, Mwanangu usome)
Tunamwomba Mungu wa mbinguni afanye njia
Mama yako kauza chapati pesa yote tumepeleka shule
(Mama yako anapenda, Mwanangu soma)

Mambo niliyoyafanya nikiwa shule sitaki hata kuyakumbuka
Moyo wangu unauma kila nikikumbuka
Maisha magumu ninayoishi uzembe wangu umechangia
Nilifanya mchezo nikiwa shule mwana
Niliona sifa daftari yangu kujisahishia
Leo hii najuta natamani kusoma
Niliona sifa kutoroka shule kupitia dirishani
Leo hii najuta natamani kusoma
Napendwa na wasupu lakini lugha inanikosa
Leo hii najuta natamani kusoma
Nikimwona mzungu kwa mbali nabadilisha njia
Naogopa asije akanisemesha 'How are You?' Na lugha sijui
Soma mwanangu, Soma wee
(Mama yako anapenda, Mwanangu soma)

Baba yako anapenda ,mwanangu usome,
mama yako anapenda ,mwanangu usome

Bony Mwaitage Feat. Bahati Bukuku

Soma Mwanangu VideoShare:

Write a review/comment/correct the lyrics of Soma Mwanangu:

0 Comments/Reviews