Chorus / Description :
Magumu shida yakupatayo ndugu, ni ya muda kidogo
Kamwe yasikutenganishe na yule, rafiki wa kweli
Hebu itegemee ahadi yake, kwamba atakuwa nawe
Hata kwenye wakati huo mgumu, mtegemee Yesu
Mambo mengi yakupata ndugu yanayokuumiza moyo
hata ukimwomba Mungu waona
kama vile amekutenga
Maisha magumu shida tupu
wapepeshwa dunia nzima
unapapasa hapa na pale
bila kupata msaada
umeanza kukata tamaa, imani yako inayumbayumba
unajisikia upweke, umeachwa kama yatima
utokako ni mbali sana, kiasi kwamba huwezi rudi
mbele huenda kunako giza, umekosa matumaini;
magumu shida yakupatayo ndugu, ni ya muda kidogo
kamwe yasikutenganishe na yule, rafiki wa kweli
hebu itegemee ahadi yake, kwamba atakuwa nawe
hata kwenye wakati huo mgumu, mtegemee Yesu
Umesongwa nazo shida nyingi, lakini mkumbuke Ayubu
alivyozidiwa nayo majaribu, akasimama imara
japo yako imefanywa wimbo, nao waumini wenzako
sawa na wale marafiki za, Ayubu walivyomcheka
Usiiruhusu shida yako, kukunyakua mkononi mwa bwana
jibu lako ni yeye pekee, tegemeo na kimbilio
hata wenzako wakutenge, vumilia utayashinda ndugu
jipe moyo mtetezi yupo, magumu atarahisisha;
Magumu shida yakupatayo ndugu, ni ya muda kidogo
kamwe yasikutenganishe na yule, rafiki wa kweli
hebu itegemee ahadi yake, kwamba atakuwa nawe
hata kwenye wakati huo mgumu, mtegemee Yesu
Umeanza kukata tamaa, imani yako inayumbayumba
unajisikia upweke, umeachwa kama yatima
utokako ni mbali sana, kiasi kwamba huwezi rudi
mbele huenda kunako giza, umekosa matumaini
usiiruhusu shida yako, kukunyakua mkononi mwa bwana
jibu lako ni yeye pekee, tegemeo na kimbilio
hata wenzako wakutenge, vumilia utayashinda ndugu
jipe moyo mtetezi yupo, magumu atarahisisha
Magumu shida yakupatayo ndugu, ni ya muda kidogo
kamwe yasikutenganishe na yule, rafiki wa kweli
hebu itegemee ahadi yake, kwamba atakuwa nawe
hata kwenye wakati huo mgumu, mtegemee Yesu