Eunice Njeri - Baba Natamani Kuwa Nawe

Chorus / Description : Natamani, Baba natamani kuwa nawe
Kuishi nawe kukaa nawe, natamani
Yesu wewe wanitosha, Bwana wangu nakutamani

Baba Natamani Kuwa Nawe Lyrics

Natamani, Baba natamani kuwa nawe
Kuishi nawe kukaa nawe, natamani
Yesu wewe wanitosha, Bwana wangu nakutamani

Baba natamani uwe wangu niwe wako
Chote kilicho changu kiwe ni chako pia
Upendo wako kwangu Yesu ni kama moto
Nimekukimbilia nisiabike milele lee Eh Baba

Baba natamani kuwa nawe
Kuishi nawe kukaa nawe, natamani
Yesu wewe wanitosha, Bwana wangu nakutamani

Baba nimeona upendo wako sio kwa mbali
Moyo wangu wafurahi ndani ya moyo wako
Nitakuinua umekuwa mwema kwangu
Pokea sifa Wewe umekuwa mwema kwangu, wewe mwema

Baba natamani kuwa nawe
Kuishi nawe kukaa nawe, natamani
Yesu wewe wanitosha, Bwana wangu nakutamani

Nitakuita hadi moyo wangu uzimie
Uniongoze kwenye mwamba ulio juu zaidi yangu
Nitakuita Bwana wangu unisikie
Ombi langu sifa zangu kilio changu
Ninapoomba (wanisikia eeh), Ninapoimba (wanisikia eeh)
Ninapolia mimi (wanisikia eeh), Ninapokuita, wanisikia eeh

Baba natamani kuwa nawe
Kuishi nawe kukaa nawe, natamani
Yesu wewe wanitosha, Bwana wangu nakutamani

Baba Natamani Kuwa Nawe Video

  • Song: Baba Natamani Kuwa Nawe
  • Artist(s): Eunice Njeri


Share: