Chorus / Description :
Nitaifanya milima tambarare
Nitayafanya mabonde yote yajae
Ntanyosha sawa njia zote
Wanadamu tutauona eeh
Giza mbele na mauti nyuma
Pande zote huo umeshindwa kwamba nini
Pesa hakuna mali umenyang'anywa
Wamekukimbia uliowategemea
Nasikia sauti kilio cha Yesu
Njooni kwangu mlio na mizigo
Nitawapumzisha hakuna kilio tena
Nitawapumzisha wataimba haleluya
Nitaifanya milima tambarare
Nitayafanya mabonde yote yajae
Ntanyosha sawa njia zote
Wanadamu tutauona eeh
Ntaifanya mambo yote mapya eeh
Tazama natenda kitu kipya leo
Imba kwa shangwe wewe uliye tasa
Shangilia sana wewe uliye tasa
Panua nafasi imani mwako
Tandaza pazia hapo unapoishi
Utapanuka kila upande
Wazawa wako watamiliki mataifa
Sema Bwana
Nitaifanya milima tambarare
Nitayafanya mabonde yote yajae
Ntanyosha sawa njia zote
Wanadamu tutauona eeh
Unaweza Yesu wewee, Mungu wangu unaweza
Mungu wangu wewe, Unaweza
Hakuna linalikushinda unaweza
Yesu wee, Yesu wee, Unaweza
Jehovah Shammah, Unaweza
Jehovah Rapha, Unaweza
Jehovah Nissi Unaweza
Elshaddai Unaweza