Chorus / Description :
Uwanene watu wenu maneno mazuri
Uwabariki kwa usemi uko mtaani
Wanapopata matatizo uumie nao
Na wakati una mazuri ufurahi nao
Mmekata kusimulia wema wangu mimi
Japo mwayajua mmenyamaza
Mko tayari kuelezea ubaya wangu mimi
(repeat)
Mliyahesabu makosa ya mtu
Mkaacha wema nilowatendea
Wala hamjali ntaumia vipi
Kwa kauli zenu mliosema
Uwanene watu wenu maneno mazuri
Uwabariki kwa usemi uko mtaani
Wanapopata matatizo uumie nao
Na wakati una mazuri ufurahi nao
Furahi pamoja na wanaofurahi
Lieni pamoja na waliao
Mkubali kushugulishwa na mambo manyonge
Msiwe wa kujivuna
Msimlipe mtu ovu kwa ovu
Anagalieni yaliyo mema machoni pa watu wote
Chozi la aliaye kwa mwenye huzuni lina thamani
Kuliko cheko la achekaye
Ajuaye huzuni la mnyonge humaanisha
Kuliko achekaye na mwenye furaha
Uwanene watu wenu maneno mazuri
Uwabariki kwa usemi uko mtaani
Wanapopata matatizo uumie nao
Na wakati una mazuri ufurahi nao